Monday, March 16, 2009

Titi la mama tamu, ingawa la mbwa

Kiswahili nakienzi
Lugha ya mama na baba,
Daima waongoza.

Mie sijatoka Uswahilini, lakini Mswahili hata hivyo. Kazaliwa katika nchi iliyo na lugha asilia za kiafrika zaidi ya arobaini. Kiswahili kikawa chombo mufti cha mawasiliano. Ninaweza kusema kwa uhakika nilikielewa Kiswahili fika kabla ya lugha ya mama.

Jameni tusiusahau urithi wetu Wakenya
Kiswahili tukienzi.

Titi la mama tamu ingawa la mbwa.

-Ferdinand Mwongela

No comments: