Kutoka kileleni mie nalia
Namwita anisike mpenzi mama
Kutoka mvunguni nanung'unika
Kiashirai nakitafuta.
Nielekeze ewe kipenzi
Mkono nishike nipate kuishi.
tateseka hadi lini?
Pa kuzaliwa sikuwa mwamuzi.
Nyumbani ni nyumbani ingawa pangoni
Nyote mlioko nisikizeni
Kilio changu kingalipo
Popote hamwendi.
Nitasimama kidete
Changu nikichukue
Kwani changu chetu
Na chako chako!
Afrika mamaaaa!
By Ferdinand Mwongela
No comments:
Post a Comment